Hivi karibuni mwanamuziki mahiri wa muziki wa Rap nchini Marekani Chris Bridges maarufu kama LUDACRIS alitoa msaada wa magari 20 kwa watu mbalimbali wenye shida. Msaada huo ulitolewa kupitia NGO aliyoianzisha inayojulikana kama THE LUDACRIS FOUNDATION. Msaada huo ulitolewa kwa njia ya shindano ambapo mshiriki alitakiwa kuelezea ni kwa nini anastahili kupewa gari hilo kwa kuelezea matatizo anayokutana nayo kwa kutokuwa na gari katika shughuli zake za kila siku.Msanii huyo mwenye umri wa miaka 31 wakati akilielezea shindano hilo alisema "People are getting laid off, and now are looking for jobs;To be efficient, you need some transportation of your own to get there. That's why I wanted to give back to those who need it". Msaada huo ulihusisha mafuta ya gari kwa siku 30 na washindi walitakiwa kujigharamia usajili, kodi na bima.
Ludacris akiwa na Mwanadada Rosario Dawson wakati wa utoaji wa tuzo za MTV MOVIE AWARDS 2006
Nafikiri hili litakuwa somo kubwa sana kwa wasanii wa bongo na Afrika Mashariki kujitolea kwa mashabiki wao kiasi cha mapato wanachopata. Hiyo haimaanishi kuwa nao watoe magari 20 kama alivyofanya Ludacris ila wanaweza kutoa chochote kwa yatima, masikini wasiojiweza na wagonjwa wasio na msaada. Sidhani kama kweli watalalamika kuwa wanachopata ni kidogo hakiwezi kutosha kutoa msaada,si kweli kwa sababu starehe ambazo baadhi yao wanazifanya zinadhihirisha kuwa fedha ipo ingawa sio kivile. Kutoa msaada katika jamii ni njia nzuri sana ya kujitangaza na ni falsafa ya kisasa ambayo watu wengi wanaitumia kama Waingereza wanavyoita "Societo-Marketing philosophy". Kwa kufanya hivyo wasanii wa bongo na Afrika Mashariki wataheshimika sana na muziki wao utapendwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
yes ni ukweli,lakini nawewe jiulize kwa nafasi yako ktk jamii unwasaidia wasiojiweza usije ukawa unapinga ufisadi wakati kumbe nawewe ni fisadi
ReplyDeleteOn my side,mimi sio employed and dats Why bado cjaweza kuwasaidia maskini na jamii ikanitambua but i promise to do so soon after gettg my first job appointment........ Lakini unataka kujifanya hujui kuwa huwa nakusaidia au mpaka niwape msaada watu wengine ndo ujue kuwa kweli nasaidia. Acha jeuri ukifulia ntakuwa sikutoi....Ha Ha Ha Am joking mjomba ila ukipata chochote wasaidie maskini!
ReplyDelete