Tuesday, September 1, 2009

DUH CHRIS BROWN ...... MPAKA HURUMA!


Mwanamuziki maarufu wa RnB duniani Chris Brown anajuta kugombana na bado anampenda mpenzi wake wa zamani ambae pia ni mwanamuziki maarufu Rihanna. Hivi karibuni chris brown alinukuliwa akisema,"I guess that night is just one of those nights I wish I could just take back, and I really regret and I feel totally ashamed of what I did." , Hiyo ilikuwa wakati akihojiwa na mtangazaji wa CNN Larry King siku ya Jumatatu 31 Agosti 2009.

Katika mahojiano hayo ambayo yanatajiwa kurushwa hewani siku ya Jumatano ya wiki hii,Chris brown alitumia muda mwingi kukanusha taarifa kwamba zilizotolewa kwamba yeye hakumbuki nini kilitokea siku alipompiga mpenzi wake ( wakati huo akiwa Rihanna),Taarifa ambazo zimesambazwa na kuenezwa sana huko unyamwezini na chombo kimojawapo cha habari ambacho hawakuelewana siku kilipomfanyia mahojiano siku za nyuma.

Chris brown alitumia pia muda huo kuwaomba msamaha watu wote waliochukizwa na tukio hilo,akiwemo kipenzi chake cha wakati huo Rihanna. Mwanamuziki huyo alisema," As I have said several times previously, I am ashamed of and sorry for what happened that night and I wish I could relive that moment and change things, but I can't. I take full responsibility for my actions. What I have to do now is to prove to the world that this was an isolated incident and that is not who I am, and I intend to do so by my behavior now and in the future."

Chris Brown na Rihanna waligombana mwezi Februari mwaka huu kwenye gari wakati wakielekea kwenye party ya maandalizi ya utoaji wa tuzo za Grammy huko Marekani. Kutokana na tukio hilo,Rihanna alimfungulia kesi Chris Brown ambayo hukumu yake imetolewa wiki iliyopita. Mojawapo ya adhabu alizopewa Chris Brown ni kutokuwa karibu na Rihanna katika kipindi chote atakachokuwa anatumikia kifungo hicho.


No comments:

Post a Comment