Wednesday, September 30, 2009

NJIA 4 ZA KUKWEPA UNENE BILA KWENDA GYM.......!

Watu wengi wanaupenda uwembamba lakini hawajui watumie njia gani ili kupunguza unene. Naposema hivi baadhi ya watu watakuwa wanashangaa kwa nini watu hawaupendi unene wakati wenyewe wanautafuta kwa hali na mali lakini hawaupati, sitanii hata kidogo kama unabisha muulize kijana wangu Sayduu au Dunia wanaotafuta ukibonge ili wawe kama Manase.

Unene mara nyingi ni hatari kwa afya zetu kwa sababu unaambatana na magonjwa kama ya Moyo na Kisukari wakati mwingine, pia uchovu wa mara kwa mara na hivyo kushindwa kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu. Zifuatazo sasa ni njia za kumfanya mtu mnene kuwa mwembamba na kinyume cha hapo zinaweza kumfanya mtu kuwa mnene;

1. KUTEMBEA HARAKA HARAKA. Hii ni njia rahisi zaidi ya kupunguza unene kwa sababu hauhitaji muda wa ziada kuifanya kazi hiyo bali ni muda uleule wa kawaida unaotembea ndio utakaokusaidia kupunguza unene. Unapokuwa unatembea jitahidi kuwa speed hata kama hauhitaji haraka ili kuchoma kama Calories 50 hivi za mwili.

2.TUMIA MWILI WAKO KUZUIA VITU. Unaweza kutumia mwili sukuma ukuta au kusukuma seat ya gari lako kwa kutumia mwili hasa unapokuwa kwenye foleni ya magari. Pia unaposoma gazeti nyumbani jaribu kukaa chini na kutengeneza Shepu ya V flani hivi. Hiyo vile vile inasaidia kuchoma Calories na kupunguza mwili.

3.MAZOEZI MADOGOMADOGO ASUBUHI AU JIONI. Fanya vijizoezi vidogo vidogo asubuhi au jioni hasa kabla hujaenda kuoga. Mazoezi hayo ni kama kusimama na kukaa, kuchuchumaa na kusimama ukiwa umeweka mikono kisogoni na mazoezi mengine nje ya hayo.

4.KUPUNGUZA MATUMIZI YA LIFT. Jitahidi kutumia lift pale ambapo unapanda ghorofani hasa kama unapokwenda hapazidi ghorofa ya 4. Hiyo itakusaidia kwa kiasi kikubwa kufanya mazoezi bila kutumia muda na gharama zozote za gym.

HIzo ni njia kubwa zinazoweza kutumika kupunguza unene kiurahisi lakini kuwa makini na aina ya lishe unayotumia kwa sababu la sivyo utakuiwa unafanya kazi ya kupunguza na kuongeza mwili kwa wakati mmoja na hivyo matokeo ya kupungua kwa mwili kutoonekana......... I wish u all the BEST.

No comments:

Post a Comment