1.Lil'Wayne.
Jina lake halisi anaitwa Dwayne Michael Carter Jr. Alizaliwa tarehe 27 September 1982 na kukulia huko New Orleans, Los Angelos. Baadae alijiunga na lebo ya Cash Money Records,Ambayo ilimuwezesha kutoa album yake ya kwanza iitwayo Get it How U live (1997) akiwa na kundi la Hot Boys na yeye akiwa kijana mdogo kuliko wote. Albamu yake ya kwanza kama solo artist aliitoa mwaka 1999 na iliitwa The block is hot lakini albamu iliyompa umaarufu zaidi ni albamu yake ya "The Carter III (2007)" ambayo ilikua na vibao kama "A milli" na "Lollipop".
2.Beyonce
3.Lady Gaga
4.Eminem
Jina lake halisi anaitwa Marshal Mathers na alizaliwa huko St. Joseph, MO karibu na Kansas City. Alianza kurap akiwa na umri wa miaka 14 wakati huo akijulikana kama M&M. Alibadili jina baadae na kujiita Eminem linalojulikana mpaka sasa. Alipata taabu sana kukubalika kwa sababu ya kuwa rapa Mweupe ukizingatia kuwa most of the rappers were Black American. Hata hivyo alikuja kukubalika kwa kasi kutokana na nyimbo zake zinazoponda watu baada ya kutoa single yake ya kwanza mwaka 1995. Muda mwingi wa uanamuziki wake amekuwa akiutumia na D12,kundi la vijana 6 ambao wamekuwa wakishirikiana ingawa wanafanya muziki kama solo artists. Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu ni pamoja na We made U,The real slim Shady, Without me na Loose yourself.
5.Michael Jackson
6.Britney Spears
Alizaliwa tarehe 2 Desemba 1981 katika mji mdogo wa Kentwood uliopo Los Angelos. Alianza kupafomu kama muimbaji na dancer katika umri mdogo. Baadae akiwa na umri wa miaka 15 alihamia New York ambapo alichukuliwa na Jive records. Alitoa single yake ya kwanza 1998 iliyoitwa " Baby one more time" chini ya Jive records. Single hiyo ilimsaidia kuitangaza vyema albamu yake ya kwanza aliyoitoa mwanzoni mwa mwaka 1999. Albamu hiyo ilipoanza kuchuja alitoa single nyingine iliyoitwa " Oops.....! I did it again" mwaka 2000 na mwaka huo huo alianza uhusiano na mwanamuziki Justin Timberlake uliodumu mpaka mwaka 2002. Uhusiano huo wa kimapenzi kati yake na Justin Timberlake ulitangazwa sana na vyombo vya habari kiasi cha kumpa umaarufu mkubwa. Mwaka 2004 alifunga ndoa na kijana Kevin Federline ambae alikuwa stage dancer,ndoa iliyosababisha kuzaliwa watoto wawili,mmoja Septemba 2005 na mwingine 2006. Baada ya kujifungua mtoto wa pili,Britney Spears alimtaliki Federline. Mwezi November 2008 alitunukiwa tuzo ya albamu bora ya mwaka na MTV Europe Music Awards,albamu ambayo ilikuwa na wimbo matata unaopendwa mpaka leo hii wa "Womanizer". Nyimbo nyingine zilizompa umaarufu ni pamoja na Me against the music, My prerogative, Toxic na Slave 4 U.
7.Miley Cyrus
Jina lake halisi anaitwa Destiny Hope Cyrus . Alizaliwa 23 November 1992 na wazazi ambao ni waigizaji hasa baba yake aitwaye Billy Ray Cyrus. Kutokana na muda mwingi kutabasamu wakati akiwa mtoto alipewa jina la utani Smiley,jina ambalo baadae lilifupishwa na kuwa Miley. Umaarufu wake ulianza mwaka 2006 as a star of the Disney Channel Television series Hannah Montana. Hili ni jina geni sana hapa nyumbani Tanzania hasa kwa watu wasiofuatilia kiundani sanaa ya Marekani
Aliendelea kujipatia umaarufu mkubwa kwa kuigiza huku akijifunza kuimba. Mpaka muda huu ninapokuletea hbari hizi,Miley Cyrus ni mwigizaji na mwimbaji mzuri anayejulikana sana huko marekani na hapa nyumbani kwa wale wafuatiliaji wazuri wa filamu na wasanii wa huko mbele akiwa among "the Cheetah girls". Baadhi ya nyimbo zake ambazo zinasikika kama soundtracks kwenye filamu zake ni The Best of Both Worlds na If We Were a Movie.
8.Shakira
Jina alilopewa na wazazi wake ni Shakira Isabel Mebarak. Alizaliwa February 2, 1977 katika familia ya kimaskini huko Barranquilla, Colombia. Baba yake ana asili ya Lebanon wakati mama yake ni mwenyeji wa Columbia. Aliandika wimbo wake wa kwanza akiwa na miaka 8, alipofikisha umri wa miaka 10 akaanza kushiriki mashindano ya uimbaji na akiwa na miaka 11 alianza kujifunza kupiga gitaa. Alitoa albamu yake ya kwanza mwaka 1991 katika studio za Sony Columbia iliyoitwa "Magia( Magic)", ingawa haikumtambulisha kimataifa lakini ilimfanya awe juu huko kwao. Mwaka 2006 alitoa albamu ambayo ilikuwa na wimbo wa "Hips dont lie", wimbo uliompa umaarufu mkubwa sana duniani. Mwaka jana 2008 alisaini mkataba wa miaka 10 na Live Nation, mkataba uliomuwezesha kuwa mwanamuziki wa kike wa 4 anayelipwa zaidi kihistoria. Sasa hivi ameshakamilisha albamu yake ya "She wolf" ambayo inategemewa kutoka October mwaka huu na itakuwa albamu yake ya 3 ya Kiingereza.
9.Led Zeppelin
Hili lilikuwa ni kundi la muziki laini lililoundwa mwaka 1967 likijulikana kama Yardbirds. Lilikuwa linaundwa na watu wanne ambao walikuwa wakibadilika badilika. Mwezi Oktoba 1968 lilianza rasmi kutumia jina la Led Zeppelin na mwezi huohuo lilitoa albamu yao ya kwanza ambayo ilirekodiwa ndani ya masaa 30. Mwishoni mwa mwaka 1968,bendi hiyo ilisaini mkataba na Atlantic Records ambao uliiwezesha kufanya matamasha mengi huko Marekani na Uingereza. Waliendelea kujitangaza zaidi na kufanya kazi kama bendi mpaka 25 Septemba 1980 ambapo mwanamuziki mmoja anayeunda kundi hilo, John Bonham alipokutwa amefariki kitandani kwake huku akiwa ametapika baada ya kushinda siku nzima anapiga ulabu na kutangaza kuvunja kundi hilo Desemba 1980. Baada ya hapo waliendelea kufanya kazi kama solo artists lakini wakishirikiana wakati mwingine na miaka ya 90 walikuwa wakiungana na kufanya kazi pamoja. Ki2 kinachofurahisha kuhusu kundi hili ni kwanza, kutokuwa karibu na vyombo vya habari na hivyo muda pekee wa kujua taarifa zao ni kununa albamu na kuhudhuria maconcert waliyokuwa wakiyaandaa. Pili, kutotoa single za hits katika albamu zao bali kutoa albamu pekee. Ni kundi ambalo litakumbukwa sana huko marekani na nchi za Ulaya Kwa kazi nzuri walizozifanya.
10.Rihanna
Jina alilopewa na wazazi wake ni Robyn Rihanna Fenty. Alizaliwa February 20, 1988, huko Saint Michael, Barbados. Alitoka kimuziki kiukweli kweli mwaka 2005 kwa kibao chake cha "Pon De Replay" na baadae kutamba na vibao viwili, kimoja katika kila mwaka uliofuatia "S.O.S." mwaka 2006; "Umbrella" mwaka 2007 na "Disturbia" mwaka 2008. Alitoa albamu mbili ambazo hata hivyo hazikuvuma sana lakini albamu yake ya tatu "Good Girl Gone Bad (2007)", ilimpaisha sana katika chati za dunia na kumfanya kuwa maarufu sana duniani. Mojawapo ya mambo yaliyomuongezea sana umaarufu ni pamoja uhusiano wa kimapenzi na jay Z, uhusiano ambao ulitangazwa sana na vyombo vya habari ulimwenguni. Nyimbo zilizompa umaarufu na zinazoendelea kependwa mpaka leo hii ni pamoja na "Umbrella,Take a Bow, Disturbia,Unfaithful, If It's Lovin' That You Want na Rehab" unaokimbiza kitaa.
Hao ni mastaa 10 maarufu zaidi duniani lakini idadi ikiongezeka na kuwa mastaa 20, wafuatao wataongezeka; Paramore(11), Taylor Swift (12), Black Eyed Peas (13), Jay Z(14), Mariah Carey (15), 50 Cent (16), Notorious B.I.G (17), Jonas Brothers(18), Akon (19) na Pussycat Dolls (20).......................Tchaooooooooooooooo!
No comments:
Post a Comment