Thursday, September 3, 2009

HAPPY BIRTHDAY MUGIZI JOAKIM (ENGINEER)........!

Kati ya siku ambazo nilifurahi,basi jana ni siku mojawapo kwa sababu kijana wangu, ndugu yangu, college mate wangu na kaka yangu Expected engineer Mugizi alikuwa anatimiza robo (1/4) karne tokea alipozaliwa. Ilikuwa ni furaha sio kwangu tu bali kwa wale wote ambao walihudhuria ile party fupi ya kumpongeza ndugu yetu huyo.Mojawapo ya watu waliokuwa na furaha kama mimi ni manase a.ka. Mporopori ak.a Mtabe, Nelson a.ka. Mandela, Addo, Aggrey, Jesca, Hadija na wengine wengi ambao walikuwepo siku hiyo ya jana.



Kwa niaba yake natumia nafasi hii kuwashukuru wote waliohudhuria sherehe hiyo ingawa najua wengi walikuwa wamebanwa na kazi za hapa na pale na wengine walikua wachoka na kazi ukizingatia wengi wetu tupo field na jana ilikuwa siku ya kazi. Tunaomba muendelee na moyo huo huo na nyie pia mnapopata nafasi msisahau kutualika ili 2enjoy nanyi.



Kwa ufupi tu, MUGIZI JOAKIM alizaliwa tarehe 2 Septemba 1984 huko kanda ya Ziwa, kukulia huko ambako pia alisoma shule ya msingi na baadae alijiunga na Bwiru boys Sec. School kwa masomo ya sekondari. Alifanikiwa kulipiga pepa fresh na kufanikiwa kujiunga na Pugu high shool mchepuo wa PCM ambapo alifanikiwa kupasuka ile mbaya. Performance yake katika mtihani wa kidato cha sita ilimuwezesha kugombaniwa na vyuo mbalimbali maarufu hapa duniani ambapo chuo kinachoheshimika Africa kwa taaluma na ukombozi wa bara la Afrika, Chuo kikuu cha Dar Es Salaam kilifanikiwa kumkamata ili awe mwanafunzi wake. Mpaka muda huu ninapoongea na wewe,kijana huyu ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu pale College of Engeneering and Technlogy maarufu kama COET katika chuo hicho maarufu zaidi Africa ak.a MLIMANI akichukua Civil Engineering.

5 comments:

  1. dah hata kunshtua kwel mi si m2 wa karib kwen

    ReplyDelete
  2. kwanza hongera sn kwa kuanzisha hii blog najua sio kazi rahisi cse it take time 2 deal with it,im marketer by nature ukiplus na miujuzi yw kanje ya marketing ninaahid kulitangaza hili blog kwa kasi sana.

    ReplyDelete
  3. ni vijana wachache sn wenye utamadun wa kufanya birtday party,ktk nchi yetu hususan ktk bala letu la africa, hivyo namim mporipori naungana kumpongeza mugiz au VITA NI VITA MURA.SASA hii ni challenge kwako nawewe km hujawah kucelebrate hii kitu ufanye hivo mimi mzee wa mausia ntaisimamia mpaka mwisho na nitasherekea ile mbaaaaaaayyyyyyyyyyyaaaaaa!

    ReplyDelete
  4. nina matatizo mengi ktk mapenzi?nahitaji ushauri wako mtaalaamu. nakosa furaha ya mapenzi kwani naona kama mpenzi wangu hana mapenzi ya dhati nami

    ReplyDelete
  5. Pole sana ndugu yangu yangu mwenye matatizo ya mapenzi, Usihofu kabisa matatizo yako yameisha. Lakini kabla sijakupa ushauri ni vema basi ukanambia ni matatizo gani yanayokusibu ili iwe rahisi kudeal nayo na kukupa ushauri ambao ni CONSTRUCTIVE.

    ReplyDelete