Friday, September 18, 2009

CHRIS BROWN AANZA KUTUMIKIA ADHABU.

Mwanamuziki Chris Brown ambaye hivi karibuni alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mi5 na kufanya shughuli za kijamii kwa kosa la kumpiga mpenzi wake wa wakati huo Rihanna, ameanza rasmi kazi ya kufanya shughuli za kijamii kwa kufanya usafi katika maeneo ya Richmond huko Virginia. Chris Brown alianza rasmi kazi hiyo siku ya J'tano wiki hii, kazi ambayo itachukua muda wa siku 180.

Vyombo mbalimbali vya habari na watu walikuwa wakishuhudia Chris Brown akifanya kazi hiyo huku akiwa kavaa mavazi kama mtu wa hali ya chini. Mavazi ambayo aliyavaa siku hiyo ni Jeans nyeusi, Vest nyeupe, kofia nyekundu ya wacheza baseball na Vest kama la traffic lenye rangi ya njano na orange pamoja na Gloves kubwa. Wakati huohuo,Chris Brown kaomba ulinzi kutoka Polisi wa Richmond ambao watakuwa na jukumu la kumlinda kipindi chote ambacho atakuwa anatumikia adhabu hiyo na ulinzi ambao yeye mwenyewe ataugharamia.

Picha ya Chris Brown akifanya kazi za kijamii kama inavyoonekana kwenye website yake ikiwa imeambatana na maneno yenye busara yasemayo," Stop and think back to the last time you accepted responsibility for something. Undertaking responsibility for each one of your actions is a difficult task but by admiting your mistakes you are taking your life to a higher level of accountability".

1 comment: