Hatimaye uhusiano wa kimapenzi kati ya The Dream na Christina Millan unaokisiwa kuanza mwezi Januari mwaka huu wa 2009 umegeuka kuwa ndoa hivi karibuni. Wanamuziki hao maarufu walifunga ndoa yao siku ya sikukuu ya Wafanyakazi huko Marekani ambayo husherekewa tarehe 4 Septemba kila mwaka. Ndoa hiyo ilifungwa Las Vegas’ Little White Wedding Chapel huko Las Vegas. Ingawa ilikuwa ni ndoa ya mastaa wakubwa wa muziki lakini ndoa hiyo ilikuwa ya gharama nafuu kwani ndoa aliyovaa bibi harusi iligharimu Dola 200 tu huku bwana harusi akipiga pamba za Dola 100 tu, kiasi abacho hata mimi mtoto wa kitaa ningeweza kuafford. Mwezi Julai mwaka huu Christina Millan alinukuliwa akisema kuwa ndoa hiyo haitakuwa kubwa pale aliposema "It’s not going to be too big.”, kitu ambacho amekifanya kama alivyoahidi.
Baada ya kuwa uvumi na sasa sio siri tena baada ya ndoa hiyo kufungwa,kwani siku moja baada ya kusherekea birthday ya Def Jam Records huko Manhattan mwezi Januari mwaka huu.... The Dream aliukana uhusiano wa kimapenzi kati yake na Christina Millan wakati wakionekana wakiwa karibu. The Dream aliuita uhusiano huo kuwa wa kibiashara na kwamba alipanga kumshirikisha katika wimbo wake ambao ungetolewa katika studio za Interscope. All in all, NAKUPONGEZA SANA na nawashauri wanamuziki wa kibongo kuoana wenyewe kwa wenyewe ili kujiongezea umaarufu na kuuza copy nyingi zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
yap, nilikuwepo ktk harusi ila sikupenda yule msimamizi wa bi harusi ile nguo aliyeivaa utafikiri tulikuwa msibani wakati ni sehem ya furaha
ReplyDeleteMmmmh acha uongo,ulikuwepo wapi wakati ulifukuzwa getini wakati unataka kuingia ndani! Tena bila kukaa karibu na mimi nadhani hata lile eneo la harusi usingesogea kwa sababu tulialikwa watu maarufu tu..................!
ReplyDelete