Monday, September 7, 2009

NI SIMBAAAAAAAAA TENA!

Haya haya ndugu zangu wa Msimbazi kama 2livyopanga mwaka huu kumaliza ligi bila kufungwa wala kutoa droo, kazi imeshaanza na raha utamu 2shaanza kupata. Mwishoni mwa wiki iliyopita chama kubwa katika Soka Afrika Mashariki na Kati,SIMBA Sports Club ilimmiminia mtoto wa Mwanza, Toto African mvua ya magoli ma3 kwa 1 (3 - 1) katika mechi iliyofanyika siku ya Jmosi ya tarehe 5 Septemba 2009 katika uwanja wa Uhuru,jijini DSM. Magoli hayo yalifungwa na washambuliaji hatari wa kimataifa Musa Hassan Mgosi, Haruna Moshi Boban na Emmanuel Okwi. Kwa ushindi huo,Simba inaongeza ligi hiyo ya Tanzania Bara ikiwa imetia kibindoni pointi 9 na magoli ya kutosha. Hekaheka za Nicco Nyagawa wa chama kubwa, Msimbazi katika mechi hiyo siku ya Jmosi katika Uwanja wa Uhuru walipomenyana na Toto African( Picha kwa hisani ya Ipp Media)

Kwa upande mwingine, ile timu nyingine inayofundishwa na profesa-feki Dusan Kondic, timu ya YANGA ilipata kipigo cha goli 1-0 ugenini huko Songea katika uwanja wa majimaji pale ilipokipiga na timu ya Majimaji ya hukohuko Songea siku ya Jumamosi iliyopita. Timu hiyo iliyomwadhibu Yanga juzijuzi ilipata kipigo cha mbwa mwizi pale ilipochabangwa goli 2 kavu na wekundu wa Msimbazi Simba.

No comments:

Post a Comment