Thursday, September 17, 2009

APATA ZALI KUTOKA U-SECRETARY MPAKA U-QUEEN!

Mwanamke mmoja,Raia wa Ghana aitwaye Peggielene Bartels na ambae anaishi na kufanya kazi huko Silver Spring,maeneo ya Washington nchini Marekani kama secretary ameukwaa U-queen nyumbani kwao ghana katika mji wa Otuam wenye wakazi wapatao 7,000 na mji huo upo umbali wa saa moja kutoka Accra ambao ni mji mkuu wa nchi ya Ghana. Mwanamke huyo alikuwa ni secretary katika ubalozi wa Ghana nchini Marekani uliopo Northwest Washington.

Kwa maelezo hayo mpaka hapo unaweza kuhisi labda huyo mwanamke kaolewa na King wa mji huo, La hasha si hivyo ila ni kwamba amepewa U-queen huo baada ya King wa mji huo ambae alikuwa na umri wa miaka 90 kufariki dunia na kukabidhiwa mikoba baada na michakato mirefu ya kumsaka mrithi wa kiti hicho.

Hayo yote yametokea wakati Mwanamke huyo akiwa nchini Ghana kwa likizo. Baada ya kupewa taarifa hizo, mwanamke huyo alikata kabisa kwa kuhisi hataweza kuifanya kazi hiyo ukizingatia kuwa alishazea kutumwatumwa na bosi wake kama mtu wa chini sana katika jamii. Hata hivyo jitihada zake za kukwepa jukumu hilo zimeshindikana na mpaka wakati huu huyo mwanamke ni Queen halali wa mji huo wa Otuam uliopo nchini Ghana.

As an advice,dont give up in whatever you are doing because you can know wat God has arrange for you in few days to come. May be God has planned to take you as a president,Prime Minister or General Secretary of AU or UN in 2025. Never give up, keep on struggling and wait for untold promise from God.

1 comment:

  1. lazima 2 huyo alikuwa analiwa na ................

    ReplyDelete