Friday, September 4, 2009

KESHO SOKA, BALAA................!

Kesho tarehe 5 Septemba 2009 vumbi litatimuka katika viwanja tofauti vya soka hapa Tanzania. mojawapo ya mechi ambazo zinasubiriwa kwa hamu sana ni mechi kaati ya Yanga na Majimaji na nyingine ni kati ya Watabe SIMBA na Toto African ya Mwanza. Mabinwa watetezi Yanga watapimana nguvu na Majimaji, mechi itakayopigwa katika uwanja wa majimaji,Songea. Mechi hiyo inategemewa kuwa ngumu kutokana na Majimaji kutumia uwanja wake wa nyumbani wakati Yanga akitaka kumkuta pointi mbabe wa mwaka huu Simba.

Kikosi cha timu ya YANGA


Wakati huohuo,Wababe wa ligi ya Mwaka huu SIMBA inakuwa inawafundisha soka watoto wa Toto African ya Mwanza ambao mwaka jana waliwanyima pointi pale katika uwanja wa Uhuru,maarufu kama Shamba la bibi. Mechi haina ugumu kwa Simba ingawa watoto hao wa Mwanza watakuwa na ndoto za kufanya walichokifanya mwaka jana wakati walipocheza pale jijini Mwanza.


Kikosi hatari cha timu ya SIMBA


Nafikiri kwa watu wa DSM kesho sio siku ya kukosa uwanja wa Uhuru kuwaona wababe wa soka mwaka huu watakavyokuwa wanatoa darasa kwa watoto wa Mwanza. Kwa wale watakaokuwepo Songea vile vile waende wakawashangae wazungu wa Yanga.


No comments:

Post a Comment