Haya haya wale mashabiki wa timu yenye kiwango kikubwa Africa Mashariki na Kati, timu ya Simba SC........ Ni shangwe kila upande! Unajua nini, Nilishasema kuwa kiwango cha timu ya Simba SC kimepitiliza, watu wakanambia Ooooh majungu oooooh Simba haina ki2 lakini nadhani nao sasa watakuwa wamekubali kuwa muziki wa simba hauchezeki!
Nasema hayo kwa sababu nilishasema mapema kwamba Simba SC atamrarua vibaya sana mtoto wa Kagera na kweli utabiri wangu umetimia baada ya jana,Simba kuichapa Kagera kwa 2 - 0 katika mchezo ambao ulichezwa uwanja wa Uhuru. Magoli hayo ya Simba yalifungwa na Haruna Moshi Boban katika kipindi cha kwanza na Mohamed Kisujo katika kipindi cha pili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment