Tuesday, September 22, 2009

RIHANNA AENDE CLUB NA SHATI LA BABAKE!


Unaweza usiamini ukaona kama nakuongopea hivi, lakini ndo ilivyotokea. Siku ya Jmosi ya tarehe 19 Septemba 2009, Mwanamuziki wa kike Rihanna alitoka na pigo matata sana wakati akienda kuspend weekend hiyo ambayo ilikuwa siku moja kabla ya sikukuu ya IDD. Hiyo ilikuwa ni pale alipokuwa akiingia katika club ya 40/40 iliyopo new York City nchini Marekani.
Rihanna alipigilia shati jeupe kubwa la kiume lililomzidi umri ambalo inasemekana kuwa ni shati la baba yake.Watu mbalimbali waliotoa maoni kuhusu uvaaji wake huo wamemsifia kuwa alipendeza na kwamba ni kawaida yake kupendeza hata kama mavazi aliyovaa ni ya ajabu.


Haya sasa mabinti wa kibongo na tabia zenu za kuiga,mvizie mdingi kaenda kuoga au yupo job afu chomoka na shati lake la kwa ofisi uzame nalo club kama hautasugua bench,I mean utacheza mwenyewe mwanzo mwisho na hakuna hata mwanume wa bahati mbaya atakayekusogelea labda awe ndugu yako....... Lakini natania tu, We pigilia afu ingia club Maisha au Billicanas,TUONEEE!

No comments:

Post a Comment