Wednesday, September 23, 2009

HOTTEST MCs IN THE GAME...........MTONI!

Mwezi Oktoba mwaka huu,MTV inatarajia kuwatangaza hottest MCs in the game huko Marekani ambao watatangazwa tarehe 4 Oktoba na MTV na habari zao kutolewa na MTV NEWS. Maemsii hao watapatikana kupitia kura ambazo zinazigatia vigezo vifuatavyo;

Lyrics: Uwezo wa kuandika mistari yenye mguso kwenye jamii na ambayo inaweza kukaa kwa muda mrefu bila kusahaulika.

Flow:Flow ya mistari ambayo imetulia na yenye uwezo wa kumpa mtu hamu ya kuendelea kuisikiliza.

Impact: Nyimbo zinazopigwa sana redioni au kwenye TV sio kwa mapenzi ya watangazaji bali maombi ya watu mbalimbali.

Buzz: wasanii wanaongelewa sana mitaani kutokana na nyimbo zao, wasanii ambao ni topic maofisini, mashuleni, vijiweni au sehemu mbalimbali kuokana na ubora wa nyimbo zao.

Sales: Wasanii ambao wanauza sana kazi zao kwa sababu yoyote ile hasa ubora wa nyimbo zao.

Intangible: Ile hali ya kukubalika bila sababu ya msingi, hali ambayo msanii anakubalika lakini wanaomkubali hawajui kwa nini wanamkubali.

Mpaka sasa kura za kutosha zimeshapigwa na zinaelekea mwisho lakini wasanii wa5 ambao wapo juu na inawezekana wakatengeneza Top 5 ni pamoja na;

EMINEM - 39%


RICK ROSS - 23%


50 CENT - 15%


JOE BUDDEN - 9%


LLOYD BANKS - 4%


Wengine baadhi ambao wapo kwenye hiyo list ni The Game ambae ana 2% na wengine ambao wana asilimia 1 ni Kanye West, Lil'Wayne,Soulja Boy na Drake.

Katika shindano kama hilo kwa miaka iliyopita, wasanii walioibuka kidedea ni Kanye West kwa mwaka 2008 na Lil'Wayne kwa mwaka 2007. Tuendelee kuvuta subira ili tuone kama kweli Eminem ataibuka kidedea au itakuwaje.......!

No comments:

Post a Comment