Wednesday, September 9, 2009

CHRIS BROWN NA RIHANNA KURUDIANA!

Tutakumbuka kuwa Chris Brown na Rihanna waligombana vibaya mwezi Februari mwaka huu. Ugomvi ulisababisha wapenzi hao kuachana na kufunguliana mashitaka mahakamani,mashitaka ambayo yalipelekea Chris Brown kupewa kifungo cha nje cha miaka mi5 na adhabu nyinginezo.

Tukiachana na hilo tutakumbuka kuwa mara kadhaa Chris Brown amekuwa akitamka hadharani kuwa bado anampenda mwanadada Rihanna na hajawahi kuacha kumpenda na amekuwa akiomba msamaha kwa watu wote walioguswa na tukio lile akiwemo Rihanna mwenyewe.

Habari zilizopo kitaa huko Marekani zinasema kuwa wapenzi hao wa zamani wana mpango wa kurudiana na kuwa wapenzi tena ingawa mojawapo ya adhabu ambayo Chris Brown alipewa ni kutokuwa karibu na Rihanna kwa muda wote atakaokuwa anatumikia kifungo hicho,Adhabu ambayo ilipingwa sana na Rihanna mwenyewe bila mafanikio.Ingawa haijaeleweka bado kama kifungo hicho ni ndani ya Marekani tu au hata nje ya nchi.

Mpango huo unaandaliwa kwa wawili hao kwenda kupumzika huko Acapulco, nchini Mexico kwa muda wa wiki 2 ambapo mambo yanayotegemewa kufanyika huko ni pamoja na kurakebisha tofauti zao na kuanza uhusiano mpya. Bado wapo kwenye process ya kuongea na mawakili wao kuona kama kuna uwezekano wa kukutana nje ya nchi au ile adhabu inazuia hata wakiwa nje ya nchi.

Kama kawaida yetu, sisi yetu macho tunasubiri kwa hamu kuona nini kitatokea na je, mpango huo utafanikiwa wa wawili hao kuwa wapenzi tena? Endelea kuwa pamoja nami kuona itakuwaje na kama safari hiyo ya mexico itafanikiwa......!

3 comments:

  1. rihanna na brown lazima warudiane kwan kugombana kwao hakuzuii nanii ya brown kucheza na ya mwenzake

    ReplyDelete
  2. Hujatulia wewe mtoto! Nanii ndo nini mbona hujamalizia? Au ulitaka kutukana? Km mpango wako ulikuwa huo basi tek kea coz kuna watoto kama Seiduu wanasoma blog hii.....!

    ReplyDelete