Friday, September 4, 2009

HATIMAYE MFALME WA POP DUNIANI AZIKWA!

Kile kitendawili cha lini mfalme wa Pop duniani, hayati Michael Jackson hatimaye jana kimeteguliwa baada ya mfalme huyo kuzikwa rasmi. mazishi hayo yalifanyika mida ya saa 2:30 usiku siku ya Alhamisi ya jana,tarehe 3 Septemba 2009 katika makaburi ya Forest Lawn kule Glendale, California. Mazishi hayo yalihudhuriwa na watu wachache sana hasa ndugu zake wakiwemo watoto wake wa3 , dada zake Janet and La Toya, kaka zake Jermaine and Tito, mamake Katherine na babake Joe. Pia mazishi hayo yalihudhuriwa na watu maarufu huko marekani wakiwemo Macaulay Culkin, Mila Kunis, Stevie Wonder, mke wake wa zamani Lisa Marie Presley, Corey Feldman, Elizabeth Taylor, Barry Bonds, Chris Tucker, Gladys Knight na Rev. Al Sharpton. Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Michael Jackson kabla hajazikwa

Katika mazishi hayo ambayo yalichukua muda wa kama lisaa limoja na dakika 15,mke wake wa zamani Bi. Presley alionekana akiwa na huzuni sana na pia mwanamuziki Gladys Knight aliperform wakati wa tukio hilo. Hiyo inamaliza safari ya mwisho hapa duniani ya mfalme wa pop duniani aliyefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuuteka ulimwengu kwa uimabji na uchezaji wake akiwa stejini.
Sehemu ya watu waliohudhuria mazishi ya Michael Jackson jana,Walio mstari wa mbele ni: Janet Jackson, Randy Jackson, Jackie Jackson, Tito Jackson, Jermaine Jackson and Marlon Jackson

No comments:

Post a Comment