Wednesday, September 16, 2009

OBAMA AMUITA KANYE WEST........ MJINGA!

Rais wa Marekani Mr. Barrack Obama amelaani kitendo cha Mwanamuziki Kanye West cha kumponda mwanamuziki kinda Taylor Swift pale alipokuwa akitoa shukrani kwa wageni waalikwa mara baaada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya Best Female Video. Kanye West alimnyang'anya mic Taylor Swift na kumwambia kuwa hakustahili kupata tuzo hiyo na badala yake alistahili Beyonce. Obama alimuita Kanye West "Jackass" (which means a male donkey,a contemptibly foolish or stupid person) kwa kitendo alichokifanya katika tukio la 2009 MTV Video Awards katika ukumbi wa muziki wa Radio City pale alipokuwa akiongea na mtangazaji wa kituo cha CNBC kabla ya kufanya mahojiano rasmi. Taarifa hizo zilirushwa na mtangazaji wa kituo cha ABC aliyakamata maneno hayo na kuyaweka hewani kupitia mtandao wa habari wa Twitter. Hata hivyo mtangazaji huyo aliomba msamaha kwa kitendo chake cha kuweka hewani maneno hayo ambayo yaliongelewa kabla mahojiano hayajaanza na kiutaratibu maongezi yote kabla ya mahojiano hayatakiwi kuwekwa hewani.

3 comments:

  1. huyo kijana namfeel ila kwa alivyofanya namfananisha na EGUWE MWEHUUUUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  2. Tatizo lako dogo huna technic za kuwa famous, Mchizi hata iwaje namkubali ile mbaya coz kumpa kubwa yule mtoto haimaanishi kipaji chake kimekufa! Nampa big up kwa kitendi chake cha kumuomba msamaha na dunia nzima imetambua kuwa mshikaji ana busara au unaonaje mtabe...........?

    ReplyDelete
  3. bwege ww unafanya ki2 afu unategemea kuomba msamaha no excuse hapa, sasa ukiambiwa una..... afu utaomba msamaha? jibu mwehu we sey hapa

    ReplyDelete