Friday, September 4, 2009

UHUSIANO WA MARLOW NA BESTA.........!


Hivi karibuni kulikuwa na maneno kibao kutoka kitaa hapa maskani kuwa yule bingwa wa sauti na kuimba, Msanii wa bongo fleva MARLOW ana uhusiano wa kimapenzi na msanii wa kike mwenye manjonjo mengi kwenye video zake na anayependa kuweka makazi yake kuleee Uganda mwanadada BESTA wana uhusiano wa kimapenzi. Habari hizo ziliendelea kunyetisha kuwa mwanadada BESTA ana ujauzito wa MARLOW............... Cjui miezi mingapi?


Lakini hivi karibuni walipoulizwa wahusika wamekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kueleza kuwa wenyewe ni marafiki sana ila urafiki wao ni wa kawaida na kwamba kinachowaweka karibu ni kuishi jirani. Mpaka hapo utata na kuhusu mimba inakuwaje? Marlow kasingiziwa, je mimba ya nani? Akitolea ufafanuzi kuhusu hilo,BESTA alisema hana ujauzito wowote na kwamba hizo ni habari za kizushi. Akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu hilo,BESTA alisema kuwa yeye ana mpenzi wake na Marlow vilevile ana mpenzi wake.

No comments:

Post a Comment