Wednesday, September 2, 2009

HESHIMA YA RAMADHANI!

Kati ya misingi bora ambayo waumini wa dini ya Kiislamu wamewekewa na ambao unafuatwa kikamilifu na karibia kila Muislamu,basi mojawapo ni Mfungo wa Ramadhani. Waislamu wengi hata wale wasioenda misikitini siku ya ijumaa hata moja,hujitaidi kwa kila hali kuhakikisha wanafunga mfungo wa Ramadhani na kuhudhuria swala ya Idd na wengine kutohudhuria hata hiyo swala ya Idd ingawa katika kipindi chote cha mfungo walikua wamefunga.

Kuna challenge mbalimbali ambazo Waislamu waliofunga hukutana nazo, lakini hasa ni hizi zifuatazo;

  • Challenge ya kwanza ni vishawishi ambavyo husababishwa na wale wasiofunga hasa wenye imani tofauti kama wakristo na wengineo. Hivyo vishawishi vinaweza kuwa ni kutokana na mavazi na tabia za baadhi ya watu. Kwa mfano m2 kunywa bia mbele ya mtu ammbae anapanda sana bia na hanywi kwa sababu kafunga.

  • Challenge ya pili ni Kutokuwa na ajira ya uhakika na ya kudumu kunakomsababishia m2 kufanya kazi ngumu zisizopangiliwa wakati wa mfungo na wakati mwingine kushindwa kutafuta pesa ya kuandalia futari na daku.

  • Challenge ya tatu ni kwa baadhi ya waliofunga ni kutunza nguvu na kujiandaa kutenda dhambi kwa fujo baada ya mfungo kuisha kwa kuanzia siku ya Idd yenyewe.

Hayo na mengine mengi ndia mara nyingi yanayoharibu swaumu za watu. Kwa mtazamo wangu nadhani mambo yafuatayo yakifanyika kwa uhakika,yatapunguza au kuondoa kabisa hizo challenges;

  • Kwanza ni kwa wale wasiofunga kujiepusha na tabia ya kuwatamanisha watu vi2 wanavyovipenda wakiwa hawajafunga na wao waliofunga pia kujiepusha na mazingira na wa2 kama hao kwa sababu wanaweza kuwaharibia swaumu zao.

  • Pili ni misikiti, mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi wenye uwezo kuwasaidia kuwafutarisha watu wasio na uwezo ili kuwafanya wafunge kwa amani bila kufikiria ni wapi watapata futari zao.

  • Tatu ni kwa misikiti kuendelea kuwaelimisha waumini wao wajue nini maana ya nfungo wa Ramadhani kwa uhakika ili waweze kuushika kwa uhakika na kuendelea na tabia njema hata baada ya mfungo.

Huo ni mtazamo wangu na sio lazima uwe kweli, inawezekana kuna seheu nimepindisha ukweli bila kujijua hivyo nakaribisha any form of comment au masahihisho ili kuweza kuwaweka watu sawa na kuishika Ramadhani vizuri.





1 comment:

  1. well done! ujue unapofunga kwanza unakuwa umetimiza nguzo 1 ya waislam,afu funga ni tiba kwani inakuwa inapumzisha viongo vyote ambavyo vinahusika na mmeng'enyo wa chakula ili sumu ktk mwili itoke thats y ndo mana wengine wananuka midomo, kupumzika kwa viungo unaupa mwili uwezo wa kugain nishati ya kutosha, kuwaasa waislam na wasio waislam kuendelea na matendo yanyompendezesha mungu

    ReplyDelete