Friday, September 4, 2009

KESHO SOKA, BALAA................!

Kesho tarehe 5 Septemba 2009 vumbi litatimuka katika viwanja tofauti vya soka hapa Tanzania. mojawapo ya mechi ambazo zinasubiriwa kwa hamu sana ni mechi kaati ya Yanga na Majimaji na nyingine ni kati ya Watabe SIMBA na Toto African ya Mwanza. Mabinwa watetezi Yanga watapimana nguvu na Majimaji, mechi itakayopigwa katika uwanja wa majimaji,Songea. Mechi hiyo inategemewa kuwa ngumu kutokana na Majimaji kutumia uwanja wake wa nyumbani wakati Yanga akitaka kumkuta pointi mbabe wa mwaka huu Simba.

Kikosi cha timu ya YANGA


Wakati huohuo,Wababe wa ligi ya Mwaka huu SIMBA inakuwa inawafundisha soka watoto wa Toto African ya Mwanza ambao mwaka jana waliwanyima pointi pale katika uwanja wa Uhuru,maarufu kama Shamba la bibi. Mechi haina ugumu kwa Simba ingawa watoto hao wa Mwanza watakuwa na ndoto za kufanya walichokifanya mwaka jana wakati walipocheza pale jijini Mwanza.


Kikosi hatari cha timu ya SIMBA


Nafikiri kwa watu wa DSM kesho sio siku ya kukosa uwanja wa Uhuru kuwaona wababe wa soka mwaka huu watakavyokuwa wanatoa darasa kwa watoto wa Mwanza. Kwa wale watakaokuwepo Songea vile vile waende wakawashangae wazungu wa Yanga.


Top 5 World's Happiest Cities

Most of the Tanzanians have little or no money and therefore they try all they can to avoid luxury expenditures. One of those luxury expenditures is travelling in different places and that's why we have a lot of national parks, games reserves and other tourist attractions but we do not know them. This articles brings you the photos of the top 5 world's happiest cities so that for those who have extra cash for luxury expenditure may decide to visit them so that they can be happy. That's all from me ,just look at them;

RIO DE JANEIRO,BRAZIL.






SYDNEY,AUSTRALIA




BARCELONA, HISPANIA.




AMSTERDAM,UHOLANZI.



MELBOURNE,AUSTRALIA.

HATIMAYE MFALME WA POP DUNIANI AZIKWA!

Kile kitendawili cha lini mfalme wa Pop duniani, hayati Michael Jackson hatimaye jana kimeteguliwa baada ya mfalme huyo kuzikwa rasmi. mazishi hayo yalifanyika mida ya saa 2:30 usiku siku ya Alhamisi ya jana,tarehe 3 Septemba 2009 katika makaburi ya Forest Lawn kule Glendale, California. Mazishi hayo yalihudhuriwa na watu wachache sana hasa ndugu zake wakiwemo watoto wake wa3 , dada zake Janet and La Toya, kaka zake Jermaine and Tito, mamake Katherine na babake Joe. Pia mazishi hayo yalihudhuriwa na watu maarufu huko marekani wakiwemo Macaulay Culkin, Mila Kunis, Stevie Wonder, mke wake wa zamani Lisa Marie Presley, Corey Feldman, Elizabeth Taylor, Barry Bonds, Chris Tucker, Gladys Knight na Rev. Al Sharpton. Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Michael Jackson kabla hajazikwa

Katika mazishi hayo ambayo yalichukua muda wa kama lisaa limoja na dakika 15,mke wake wa zamani Bi. Presley alionekana akiwa na huzuni sana na pia mwanamuziki Gladys Knight aliperform wakati wa tukio hilo. Hiyo inamaliza safari ya mwisho hapa duniani ya mfalme wa pop duniani aliyefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuuteka ulimwengu kwa uimabji na uchezaji wake akiwa stejini.
Sehemu ya watu waliohudhuria mazishi ya Michael Jackson jana,Walio mstari wa mbele ni: Janet Jackson, Randy Jackson, Jackie Jackson, Tito Jackson, Jermaine Jackson and Marlon Jackson

UHUSIANO WA MARLOW NA BESTA.........!


Hivi karibuni kulikuwa na maneno kibao kutoka kitaa hapa maskani kuwa yule bingwa wa sauti na kuimba, Msanii wa bongo fleva MARLOW ana uhusiano wa kimapenzi na msanii wa kike mwenye manjonjo mengi kwenye video zake na anayependa kuweka makazi yake kuleee Uganda mwanadada BESTA wana uhusiano wa kimapenzi. Habari hizo ziliendelea kunyetisha kuwa mwanadada BESTA ana ujauzito wa MARLOW............... Cjui miezi mingapi?


Lakini hivi karibuni walipoulizwa wahusika wamekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kueleza kuwa wenyewe ni marafiki sana ila urafiki wao ni wa kawaida na kwamba kinachowaweka karibu ni kuishi jirani. Mpaka hapo utata na kuhusu mimba inakuwaje? Marlow kasingiziwa, je mimba ya nani? Akitolea ufafanuzi kuhusu hilo,BESTA alisema hana ujauzito wowote na kwamba hizo ni habari za kizushi. Akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu hilo,BESTA alisema kuwa yeye ana mpenzi wake na Marlow vilevile ana mpenzi wake.

THE MOST POPULAR ARTISTS...........!

Kwa hali ya kawaida ni vigumu sana kujua kwa wakati huu ni wasanii gani wapo juu zaidi duniani, kwa sababu karibu kila mtu an preference zake ambazo ni tofauti na preference za mwingine. Hata hivyo kulingana na utafiti uliofanyika na kutolewa na website ya MTV,inaonesha kwa sasa the most 10 popular artists ni hawa hapa:

1.Lil'Wayne.

Jina lake halisi anaitwa Dwayne Michael Carter Jr. Alizaliwa tarehe 27 September 1982 na kukulia huko New Orleans, Los Angelos. Baadae alijiunga na lebo ya Cash Money Records,Ambayo ilimuwezesha kutoa album yake ya kwanza iitwayo Get it How U live (1997) akiwa na kundi la Hot Boys na yeye akiwa kijana mdogo kuliko wote. Albamu yake ya kwanza kama solo artist aliitoa mwaka 1999 na iliitwa The block is hot lakini albamu iliyompa umaarufu zaidi ni albamu yake ya "The Carter III (2007)" ambayo ilikua na vibao kama "A milli" na "Lollipop".



2.Beyonce

Jina lake halisi ni Beyonce Giselle Knowles,alizaliwa September 1981 huko Houston,Marekani. Alianza kuimba na kucheza muziki akiwa na umri wa miaka 7 huko mtaani kwao na baadae kuunda kundi la kuimba pamoja na binamu yake aitwae Kelly Rowland na maclassmates wake wengine. Baba mzazi wa Beyonce na mlezi wa Kelly, Mzee Mathew Knowles alisaini nao mkataba wa kuwa meneja wao na baadae aliamua kuacha kazi aliyokua anafanya ili atumue muda mwingi kuboresha vipaji vya vijana hao. Meneja huyo alifanikiwa kuunda kundi maarufu ambalo liliitwa Destiny Child likiwa na wadada machachari kama Beyonce,Kelly Rowland,Luckett na Roberson. Baadae ulitokea mtafaruku baina ya Luckett na Roberson kwa upande mmoja na Meneja wao, ambao ulisababisha kujitoa kwa wasanii hao wawili. Mnamo mwaka 2001, Mdada Michelle Williams alijiunga na kundi hilo kuziba nafasi ya wadada waliojitoa. Beyonce alitoa albamu yake ya kwanza iliyoitwa Dangerously in love kama Solo artist mwaka 2003 baada ya kila msanii kwenye kundi lao kuwa solo. Mwaka uliofuatia kundi lilirudi tena kutoa albamu ya mwisho waliyoiita Destiny fulfilled. Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu ni pamoja na Crazy in luv, Irreplaceable, Upgrade U, Dangerously in luv 2 and hello.


3.Lady Gaga

Lady Gaga ambae jina lake halisi ni Stefani Germanotta alizaliwa tarehe 28 March 1986 huko Yonkers,New York City marekani. Alisoma katika shule ya masista wakatoliki wa Sacred Heart na baadae alijiunga na shule ya sanaa ya Tisch ya New York University ambapo alisomea muziki akiwa na umri wa miaka 17. Mnamo mwaka 2007 alisaini mkataba na lebo ya Def Jam ambayo hata hivyo haikumpa mafanikio mpaka pale alipochukuliwa na Akon chini ya lebo ya Kon Live kwa ushirikiano na Interscope Records. Akiwa chini ya Kon Live alifanikiwa kutoa wimbo uliompa mafanikio makubwa wa Just dance ambao ulianza kupigwa redioni April 2008 hukooo Unyamwezini. Baada ya hapo anaendelea kukimbiza na wimbo wake wa Poker Face mpaka wakati huu.


4.Eminem

Jina lake halisi anaitwa Marshal Mathers na alizaliwa huko St. Joseph, MO karibu na Kansas City. Alianza kurap akiwa na umri wa miaka 14 wakati huo akijulikana kama M&M. Alibadili jina baadae na kujiita Eminem linalojulikana mpaka sasa. Alipata taabu sana kukubalika kwa sababu ya kuwa rapa Mweupe ukizingatia kuwa most of the rappers were Black American. Hata hivyo alikuja kukubalika kwa kasi kutokana na nyimbo zake zinazoponda watu baada ya kutoa single yake ya kwanza mwaka 1995. Muda mwingi wa uanamuziki wake amekuwa akiutumia na D12,kundi la vijana 6 ambao wamekuwa wakishirikiana ingawa wanafanya muziki kama solo artists. Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu ni pamoja na We made U,The real slim Shady, Without me na Loose yourself.

5.Michael Jackson

Jina alilopewa na wazazi wake ni Michael Joseph Jackson. Alizaliwa tarehe 29 Agosti 1958 katika maeneo ya Industrial Midwestern town of Gary,Indiana huko Marekani. Alianza kuimba na kudance akiwa na umri wa miaka 5 katika kundi moja na kaka zake, kundi likijulikana kama Jackson 5. Mwaka 1978,nyota ya Michael Jackson ilianza kung'ara na alionekana kama kijana mwenye kipaji kikubwa kuliko kaka zake. Kibao cha off the Wall ndio kilichomtoa kama solo artist na baadae kibao cha Thriller na the Victory tour ya mwaka 1984 ndio vilimfanya awe the biggest star in the world. Kati ya mwaka 1986 na mwaka 1999, MJ alipata mafanikio makubwa sana kiasi cha kupachikwa jina la utani la Wacko Jacko na pia kuwa named kama artist of the world na Rais George H.W. Bush wa Marekani wa wakati huo.

Kati ya mwaka 2000 na 2009, hakupata mafanikio yoyote makubwa kutokana na kuandamwa na scandals za mara kwa mara ingawa alikuwa kwenye plan za kurudi kwenye game kwa shows 5o alizotakiwa kuzifanya mwaka huu huko London,Uingereza. Unfortunately,on 25th June this year at 2.26p.m PT alifariki dunia kwa maradhi ya moyo akiwa na umri wa miaka 50. Tokea utoto wake mpaka anafariki.The late MJ ameuza zaidi ya 750 millions records worldwide na baada ya kutangazwa kifo chake, iligundulika kuwa hakika Michael Joseph Jackson was and always will be the king of pop.


6.Britney Spears

Alizaliwa tarehe 2 Desemba 1981 katika mji mdogo wa Kentwood uliopo Los Angelos. Alianza kupafomu kama muimbaji na dancer katika umri mdogo. Baadae akiwa na umri wa miaka 15 alihamia New York ambapo alichukuliwa na Jive records. Alitoa single yake ya kwanza 1998 iliyoitwa " Baby one more time" chini ya Jive records. Single hiyo ilimsaidia kuitangaza vyema albamu yake ya kwanza aliyoitoa mwanzoni mwa mwaka 1999. Albamu hiyo ilipoanza kuchuja alitoa single nyingine iliyoitwa " Oops.....! I did it again" mwaka 2000 na mwaka huo huo alianza uhusiano na mwanamuziki Justin Timberlake uliodumu mpaka mwaka 2002. Uhusiano huo wa kimapenzi kati yake na Justin Timberlake ulitangazwa sana na vyombo vya habari kiasi cha kumpa umaarufu mkubwa. Mwaka 2004 alifunga ndoa na kijana Kevin Federline ambae alikuwa stage dancer,ndoa iliyosababisha kuzaliwa watoto wawili,mmoja Septemba 2005 na mwingine 2006. Baada ya kujifungua mtoto wa pili,Britney Spears alimtaliki Federline. Mwezi November 2008 alitunukiwa tuzo ya albamu bora ya mwaka na MTV Europe Music Awards,albamu ambayo ilikuwa na wimbo matata unaopendwa mpaka leo hii wa "Womanizer". Nyimbo nyingine zilizompa umaarufu ni pamoja na Me against the music, My prerogative, Toxic na Slave 4 U.



7.Miley Cyrus

Jina lake halisi anaitwa Destiny Hope Cyrus . Alizaliwa 23 November 1992 na wazazi ambao ni waigizaji hasa baba yake aitwaye Billy Ray Cyrus. Kutokana na muda mwingi kutabasamu wakati akiwa mtoto alipewa jina la utani Smiley,jina ambalo baadae lilifupishwa na kuwa Miley. Umaarufu wake ulianza mwaka 2006 as a star of the Disney Channel Television series Hannah Montana. Hili ni jina geni sana hapa nyumbani Tanzania hasa kwa watu wasiofuatilia kiundani sanaa ya Marekani


Aliendelea kujipatia umaarufu mkubwa kwa kuigiza huku akijifunza kuimba. Mpaka muda huu ninapokuletea hbari hizi,Miley Cyrus ni mwigizaji na mwimbaji mzuri anayejulikana sana huko marekani na hapa nyumbani kwa wale wafuatiliaji wazuri wa filamu na wasanii wa huko mbele akiwa among "the Cheetah girls". Baadhi ya nyimbo zake ambazo zinasikika kama soundtracks kwenye filamu zake ni The Best of Both Worlds na If We Were a Movie.



8.Shakira


Jina alilopewa na wazazi wake ni Shakira Isabel Mebarak. Alizaliwa February 2, 1977 katika familia ya kimaskini huko Barranquilla, Colombia. Baba yake ana asili ya Lebanon wakati mama yake ni mwenyeji wa Columbia. Aliandika wimbo wake wa kwanza akiwa na miaka 8, alipofikisha umri wa miaka 10 akaanza kushiriki mashindano ya uimbaji na akiwa na miaka 11 alianza kujifunza kupiga gitaa. Alitoa albamu yake ya kwanza mwaka 1991 katika studio za Sony Columbia iliyoitwa "Magia( Magic)", ingawa haikumtambulisha kimataifa lakini ilimfanya awe juu huko kwao. Mwaka 2006 alitoa albamu ambayo ilikuwa na wimbo wa "Hips dont lie", wimbo uliompa umaarufu mkubwa sana duniani. Mwaka jana 2008 alisaini mkataba wa miaka 10 na Live Nation, mkataba uliomuwezesha kuwa mwanamuziki wa kike wa 4 anayelipwa zaidi kihistoria. Sasa hivi ameshakamilisha albamu yake ya "She wolf" ambayo inategemewa kutoka October mwaka huu na itakuwa albamu yake ya 3 ya Kiingereza.



9.Led Zeppelin



Hili lilikuwa ni kundi la muziki laini lililoundwa mwaka 1967 likijulikana kama Yardbirds. Lilikuwa linaundwa na watu wanne ambao walikuwa wakibadilika badilika. Mwezi Oktoba 1968 lilianza rasmi kutumia jina la Led Zeppelin na mwezi huohuo lilitoa albamu yao ya kwanza ambayo ilirekodiwa ndani ya masaa 30. Mwishoni mwa mwaka 1968,bendi hiyo ilisaini mkataba na Atlantic Records ambao uliiwezesha kufanya matamasha mengi huko Marekani na Uingereza. Waliendelea kujitangaza zaidi na kufanya kazi kama bendi mpaka 25 Septemba 1980 ambapo mwanamuziki mmoja anayeunda kundi hilo, John Bonham alipokutwa amefariki kitandani kwake huku akiwa ametapika baada ya kushinda siku nzima anapiga ulabu na kutangaza kuvunja kundi hilo Desemba 1980. Baada ya hapo waliendelea kufanya kazi kama solo artists lakini wakishirikiana wakati mwingine na miaka ya 90 walikuwa wakiungana na kufanya kazi pamoja. Ki2 kinachofurahisha kuhusu kundi hili ni kwanza, kutokuwa karibu na vyombo vya habari na hivyo muda pekee wa kujua taarifa zao ni kununa albamu na kuhudhuria maconcert waliyokuwa wakiyaandaa. Pili, kutotoa single za hits katika albamu zao bali kutoa albamu pekee. Ni kundi ambalo litakumbukwa sana huko marekani na nchi za Ulaya Kwa kazi nzuri walizozifanya.

10.Rihanna


Jina alilopewa na wazazi wake ni Robyn Rihanna Fenty. Alizaliwa February 20, 1988, huko Saint Michael, Barbados. Alitoka kimuziki kiukweli kweli mwaka 2005 kwa kibao chake cha "Pon De Replay" na baadae kutamba na vibao viwili, kimoja katika kila mwaka uliofuatia "S.O.S." mwaka 2006; "Umbrella" mwaka 2007 na "Disturbia" mwaka 2008. Alitoa albamu mbili ambazo hata hivyo hazikuvuma sana lakini albamu yake ya tatu "Good Girl Gone Bad (2007)", ilimpaisha sana katika chati za dunia na kumfanya kuwa maarufu sana duniani. Mojawapo ya mambo yaliyomuongezea sana umaarufu ni pamoja uhusiano wa kimapenzi na jay Z, uhusiano ambao ulitangazwa sana na vyombo vya habari ulimwenguni. Nyimbo zilizompa umaarufu na zinazoendelea kependwa mpaka leo hii ni pamoja na "Umbrella,Take a Bow, Disturbia,Unfaithful, If It's Lovin' That You Want na Rehab" unaokimbiza kitaa.

Hao ni mastaa 10 maarufu zaidi duniani lakini idadi ikiongezeka na kuwa mastaa 20, wafuatao wataongezeka; Paramore(11), Taylor Swift (12), Black Eyed Peas (13), Jay Z(14), Mariah Carey (15), 50 Cent (16), Notorious B.I.G (17), Jonas Brothers(18), Akon (19) na Pussycat Dolls (20).......................Tchaooooooooooooooo!




Thursday, September 3, 2009

HAPPY BIRTHDAY MUGIZI JOAKIM (ENGINEER)........!

Kati ya siku ambazo nilifurahi,basi jana ni siku mojawapo kwa sababu kijana wangu, ndugu yangu, college mate wangu na kaka yangu Expected engineer Mugizi alikuwa anatimiza robo (1/4) karne tokea alipozaliwa. Ilikuwa ni furaha sio kwangu tu bali kwa wale wote ambao walihudhuria ile party fupi ya kumpongeza ndugu yetu huyo.Mojawapo ya watu waliokuwa na furaha kama mimi ni manase a.ka. Mporopori ak.a Mtabe, Nelson a.ka. Mandela, Addo, Aggrey, Jesca, Hadija na wengine wengi ambao walikuwepo siku hiyo ya jana.



Kwa niaba yake natumia nafasi hii kuwashukuru wote waliohudhuria sherehe hiyo ingawa najua wengi walikuwa wamebanwa na kazi za hapa na pale na wengine walikua wachoka na kazi ukizingatia wengi wetu tupo field na jana ilikuwa siku ya kazi. Tunaomba muendelee na moyo huo huo na nyie pia mnapopata nafasi msisahau kutualika ili 2enjoy nanyi.



Kwa ufupi tu, MUGIZI JOAKIM alizaliwa tarehe 2 Septemba 1984 huko kanda ya Ziwa, kukulia huko ambako pia alisoma shule ya msingi na baadae alijiunga na Bwiru boys Sec. School kwa masomo ya sekondari. Alifanikiwa kulipiga pepa fresh na kufanikiwa kujiunga na Pugu high shool mchepuo wa PCM ambapo alifanikiwa kupasuka ile mbaya. Performance yake katika mtihani wa kidato cha sita ilimuwezesha kugombaniwa na vyuo mbalimbali maarufu hapa duniani ambapo chuo kinachoheshimika Africa kwa taaluma na ukombozi wa bara la Afrika, Chuo kikuu cha Dar Es Salaam kilifanikiwa kumkamata ili awe mwanafunzi wake. Mpaka muda huu ninapoongea na wewe,kijana huyu ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu pale College of Engeneering and Technlogy maarufu kama COET katika chuo hicho maarufu zaidi Africa ak.a MLIMANI akichukua Civil Engineering.

Wednesday, September 2, 2009

LYRICS - ONE STEP AT A TIME by Jordin Sparks.

Hurry up and wait so close but so far away
Everything that you've always dreamed of
Close enough for you to taste but you just can't touch

You wanna show the world but no one knows your name yet
Wonder when and where and how you're gonna make it
You know you can if you get the chance
In your face and the door keeps slamming

Now you're feeling more and more frustrated
And you're getting all kind of impatient, waiting
We live and we learn to take

One step at a time there's no need to rush
It's like learning to fly or falling in love
It's gonna happen and it's supposed to happen
That we find the reasons why, one step at a time

You believe and you doubt
You're confused and got it all figured out
Everything that you always wished for
Could be yours, should be yours, would be yours if they only knew

You wanna show the world but no one knows your name yet
Wonder when and where and how you're gonna make it
You know you can if you get the chance
In your face and the door keeps slamming

Now you're feeling more and more frustrated
And you're getting all kind of impatient, waiting
We live and we learn to take

One step at a time there's no need to rush
It's like learning to fly or falling in love
It's gonna happen and it's supposed to happen
That we find the reasons why, one step at a time

When you can't wait any longer
But there's no end in sight
It's the faith that makes you stronger
The only way we get there is one step at a time

Take one step at a time there's no need to rush
It's like learning to fly or falling in love
It's gonna happen and it's supposed to happen
That we find the reasons why, one step at a time

One step at a time there's no need to rush
It's like learning to fly or falling in love
It's gonna happen and it's supposed to happen
That we find the reasons why, one step at a time

HESHIMA YA RAMADHANI!

Kati ya misingi bora ambayo waumini wa dini ya Kiislamu wamewekewa na ambao unafuatwa kikamilifu na karibia kila Muislamu,basi mojawapo ni Mfungo wa Ramadhani. Waislamu wengi hata wale wasioenda misikitini siku ya ijumaa hata moja,hujitaidi kwa kila hali kuhakikisha wanafunga mfungo wa Ramadhani na kuhudhuria swala ya Idd na wengine kutohudhuria hata hiyo swala ya Idd ingawa katika kipindi chote cha mfungo walikua wamefunga.

Kuna challenge mbalimbali ambazo Waislamu waliofunga hukutana nazo, lakini hasa ni hizi zifuatazo;

  • Challenge ya kwanza ni vishawishi ambavyo husababishwa na wale wasiofunga hasa wenye imani tofauti kama wakristo na wengineo. Hivyo vishawishi vinaweza kuwa ni kutokana na mavazi na tabia za baadhi ya watu. Kwa mfano m2 kunywa bia mbele ya mtu ammbae anapanda sana bia na hanywi kwa sababu kafunga.

  • Challenge ya pili ni Kutokuwa na ajira ya uhakika na ya kudumu kunakomsababishia m2 kufanya kazi ngumu zisizopangiliwa wakati wa mfungo na wakati mwingine kushindwa kutafuta pesa ya kuandalia futari na daku.

  • Challenge ya tatu ni kwa baadhi ya waliofunga ni kutunza nguvu na kujiandaa kutenda dhambi kwa fujo baada ya mfungo kuisha kwa kuanzia siku ya Idd yenyewe.

Hayo na mengine mengi ndia mara nyingi yanayoharibu swaumu za watu. Kwa mtazamo wangu nadhani mambo yafuatayo yakifanyika kwa uhakika,yatapunguza au kuondoa kabisa hizo challenges;

  • Kwanza ni kwa wale wasiofunga kujiepusha na tabia ya kuwatamanisha watu vi2 wanavyovipenda wakiwa hawajafunga na wao waliofunga pia kujiepusha na mazingira na wa2 kama hao kwa sababu wanaweza kuwaharibia swaumu zao.

  • Pili ni misikiti, mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi wenye uwezo kuwasaidia kuwafutarisha watu wasio na uwezo ili kuwafanya wafunge kwa amani bila kufikiria ni wapi watapata futari zao.

  • Tatu ni kwa misikiti kuendelea kuwaelimisha waumini wao wajue nini maana ya nfungo wa Ramadhani kwa uhakika ili waweze kuushika kwa uhakika na kuendelea na tabia njema hata baada ya mfungo.

Huo ni mtazamo wangu na sio lazima uwe kweli, inawezekana kuna seheu nimepindisha ukweli bila kujijua hivyo nakaribisha any form of comment au masahihisho ili kuweza kuwaweka watu sawa na kuishika Ramadhani vizuri.





Tuesday, September 1, 2009

DUH CHRIS BROWN ...... MPAKA HURUMA!


Mwanamuziki maarufu wa RnB duniani Chris Brown anajuta kugombana na bado anampenda mpenzi wake wa zamani ambae pia ni mwanamuziki maarufu Rihanna. Hivi karibuni chris brown alinukuliwa akisema,"I guess that night is just one of those nights I wish I could just take back, and I really regret and I feel totally ashamed of what I did." , Hiyo ilikuwa wakati akihojiwa na mtangazaji wa CNN Larry King siku ya Jumatatu 31 Agosti 2009.

Katika mahojiano hayo ambayo yanatajiwa kurushwa hewani siku ya Jumatano ya wiki hii,Chris brown alitumia muda mwingi kukanusha taarifa kwamba zilizotolewa kwamba yeye hakumbuki nini kilitokea siku alipompiga mpenzi wake ( wakati huo akiwa Rihanna),Taarifa ambazo zimesambazwa na kuenezwa sana huko unyamwezini na chombo kimojawapo cha habari ambacho hawakuelewana siku kilipomfanyia mahojiano siku za nyuma.

Chris brown alitumia pia muda huo kuwaomba msamaha watu wote waliochukizwa na tukio hilo,akiwemo kipenzi chake cha wakati huo Rihanna. Mwanamuziki huyo alisema," As I have said several times previously, I am ashamed of and sorry for what happened that night and I wish I could relive that moment and change things, but I can't. I take full responsibility for my actions. What I have to do now is to prove to the world that this was an isolated incident and that is not who I am, and I intend to do so by my behavior now and in the future."

Chris Brown na Rihanna waligombana mwezi Februari mwaka huu kwenye gari wakati wakielekea kwenye party ya maandalizi ya utoaji wa tuzo za Grammy huko Marekani. Kutokana na tukio hilo,Rihanna alimfungulia kesi Chris Brown ambayo hukumu yake imetolewa wiki iliyopita. Mojawapo ya adhabu alizopewa Chris Brown ni kutokuwa karibu na Rihanna katika kipindi chote atakachokuwa anatumikia kifungo hicho.


BADO HAWAAMINI KIFO CHA MJ.......WACKO!


Jamaa kibao mpaka leo bado wanapinga kifo cha mfalme wa pop duniani Hayati Michael Jackson. Kulingana na habari ambazo zipo kitaa huko unyamwezini, bado daktari wake binafsi Dr. Conrad Murray yupo matatani kwa kusababisha kifo cha mfalme huyo ambae alikuwa anapendwa na watu kibao ulimwenguni. Hiyo inatokana na habari zilizopatikana kuwa huyo daktari alimpa mfalme dawa nyingi asubuhi ya siku hiyo aliyofariki na kwamba dawa za mtindo huo alikuwa akimpa mara kwa mara,inaaminika ni kila baada ya nusu saa wakati hizo dawa zinatakiwa kutolewa at least kila baada ya masaa ma4,nanukuu "At 1:30 a.m., Murray gave Michael valium. At 2 a.m., he injected him with lorazepam, and, at 3 a.m., Murray administered midzaloam". Jamaa mmoja alisikika akisema "By 10:40 a.m. the morning of Michael's death, Murray gave him propofol, which ultimately killed him". Jamaa hawezi kukwepa kifungo,unajua kwa sababu gani? Kuna habari pia zinasema "Even a person without an education in medicine would consider suspect the dosages of medicine Murray administered to Michael",kwa kauli kama hizo jamaa atapona kweli......... sijui? Labda kuwe na ufisadi mkubwa kama bongo,otherwise mmmmmmmh,hatari jamaa atanyea debe! Mfalme wa pop duniani Michael Jackson alifariki dunia Juni 25,2009 baada ya kushambuliwa na maradhi ya moyo ambayo inasemekana yalisababishwa na dawa alizopewa na daktari wake.