Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana kilianza ziara ya kuongeza idadi ya wanachama na kutanua chama kanda ya nyanda za juu kusini. Ziara hiyo ilianzia mkoani Mbeya kwa kufanya maandamano na mkutano wa hadhara.
Hivi ndivyo maandamano yalivyokua
Tofauti na wengi walivyotegemea, mkutano huo ulijaza idadi kubwa ya watu. Wengi walitegemea mkutano huo ungedoda kutokana na kuhama chama kwa aliyekua mwenyekiti wa chama mkoa wa mbeya bwana Shitambala.
Mabango yalikua ya kutoa upinzani haswa kwa vyama vingine.
Mwisho wa yote ulifanyika mkutano mkubwa wa hadhara uliohutubiwa na viongozi wa chama wa kitaifa na wa mkoa kama inavyoonekana katika picha hapo chini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment