Wednesday, December 15, 2010
Hivi Mitandao ya simu inatujali zaidi kuliko serikali yetu...?
Karibu kila mwaka mitandao ya simu Tanzania inapunguza bei za huduma zao. hii inatusaidia hata watu wa kipato cha chini kuwasiliana kiurahisi bila kudhoofisha hali zetu za kiuchumi.
Nimekua nikijiuliza kila mara, Hivi hii inamaanisha kuwa mitandao ya simu inatujali sana kuliko serikali yetu ambayo inaachia maongezeko mengi ya bei za vitu ambavyo ingeweza kuyazuia au kuyapunguza kama ongezeko la bei ya mafuta ghafi?
Naombeni mawazo yenu wadau...!?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment