Habari za kuaminika kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zinasema mwanamuziki maarufu wa Hip hop nchini Marekani Li' Wayne anatarajia kupata mtoto wa kiume kupitia kwa mpenzi wake mpya ambaye ni mwanamuziki wa RNB aitwaye NIVEA. Inasemekana kuwa mtoto huyo atakuwa ni mtoto wa tatu kuzaliwa wa Lil'Wayne ndani ya kipindi cha mwaka mmoja ambapo mtoto mmoja alipatikana mwezi Oktoba mwaka jana 2008,mwingine mwezi uliopita Septemba 2009 ana watatu anatarajia kupatikana mwezi huu.
Hata hivyo, habari zaidi zinaeleza kuwa mtoto huyo atakuwa mtoto wa nne kuzaliwa kwa rapa huyo maarufu nchini Marekani. Pia kuna tetesi kuwa kwa sasa Rapa huyo ana wapenzi wawili ambao wana mimba zake na hivyo kufanya idadi ya wanawake wanne ambao kaaza nao ingawa wawili kati ya hao hawafahamiki vizuri.
Duh hili balaa, kumbe tabia ya kuzaa hovyo hata people wa huko mbele wanayo hasa ukizingatia kuwa Lil' Wayne hafanani kabisa na tabia hiyo. Haya wale wenzangu na mimi wenye tabia ya kuiga lifestyle za wasanii wa Mtoni igeni na hilo basi tuoneee!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment